Na Mwandishi wetu.
Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu Msanii wa Filamu, Elizabeth Micheal (Lulu) kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.
Hukumu iliyosomwa na Jaji Sam Rumanyika imemtia hatiani Lulu kuwa alimuua msani mwenzake, Marehemu Kanumba bila kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 Sinza Kinondoni Dar es Salaam.
Kwa mara ya kwanza Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , lakini baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu hiyo leo.
Jaji Rumanyika anesema amemtia hatiani lulu kuuwa bila kukusudia kwa kuzingatia kifungu cha 195 cha sheria.
Upande wa Jamhuri ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba moja na marehemu na aliyekuwepo siku ya tukio, Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia hiyo ambaye aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka.
Wengine ni Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Kanumba pamoja askari ASP Ester aliyefanya upelelezi kwenye tukio hilo pamoja na kumtia mbaroni Lulu.
Lulu aambaye anatetewa na wakili Peter Kibatala, waliwasilisha mashahidi wa wawili ambao ni Lulu mwenyewe aliyehadithia mazingira ya tukio na kueleza kuwa hakuhusika kwa namna yoyote kwenye kifo cha Marehemu Kanumba.
Hata hivyo Wakili wa Lulu, Kibatala amesema wanajipanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Comments