Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuna wanachama wa vyama vya upinzani 200 ambao wameomba kujiunga na CCM.
Akizungumza leo Jumanne wakati wa kutangaza majina ya viongozi wa mikoa na kitaifa walioomba nafasi mbalimbali za uongozi CCM, Polepole amesema wapinzani walioomba kujiunga na chama hicho wamo wabunge na wenyeviti.
Amesema sababu waliyotoa ya kutaka kuhamia CCM ni kutokana na chama hicho kushughulika na matatizo ya watu.
Polepole amesema chama kimewapokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani.
Amewataja wanachama hao kuwa ni Samson Mwigamba, Albert Msando na Profesa Kitila Mkumbo kutoka ACT-Wazalendo. Wengine na Lawrence Masha na Protobas Katambi wa Chadema.
"Tutawajulisha siku tutakapowapokea wanachama hawa wapya," amesema.
Source:Mwananchi
Comments