Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauniwatembelea mpaka unaotenganisha Tanzania na Kenya
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) wakiangalia jiwe la mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda, wilayani Tarime ambapo upande wa pili ni Kaunti ya Migori nchini Kenya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala(watatu kulia),akizungmza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wakielekea kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda,Wilayani Tarime.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea alama ya Mpaka unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda wilayani Tarime.Wengine ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.
Comments