Mbwana Samatta(PICHA NA MTANDAO)
Mchezaji machachari klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania TAIFA STARS,Mbwana Samatta ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram kuwa hali yake inazidi kuendelea kuwa vizuri.
“Napenda kuwajulisha kuwa, upasuaji wangu umeenda vizuri. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, timu ya madaktari pamoja na mashabiki wangu.”
“Nimepokea meseji nyingi sana kutoka sehemu tofauti duniani na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa meseji na Dua zenu.”ameandika Samatta kwenye ukurasa wake wa instagram
Samata alipata jeraha la kuumia goti novemba 4,2017 wakati akiitumikia klabu yake ya KRC Genk.
Comments