Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya “Zilipendwa”
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa” Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo.
“Unaweza
kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba
wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya
haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye
kazi mkubaliane”
“Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja
kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili
kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi
yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la
kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu
ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” –
Mngereza
Comments