STAA wa kike, Serena Williams mwenye miaka 36, amefanikiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi, Alexis Ohanian mwenye miaka 34.
Wawili hao walivalishana pete ya uchumba Desemba, mwaka jana na kukaa miezi 11 kabla ya kuhalalisha uhusiano wao kwa kufunga ndoa.
Katika sherehe hiyo, mastaa mbalimbali walihudhuria wakiwemo Beyonce, Kim Kadarshian, Eva Longoria na Caroline Wozniacki.
Sherehe ilifanyika katika jiji la New Orleans huku wawili hao wakiwa tayari wameshapata mtoto mmoja.
Comments