Rais Robert
Mugabe wa Zimbabwe amekubali kujiuzulu kwa masharti mawili.
Masharti hayo
ni kuwekewa kinga ya kutoshitakiwa yeye na mkewe Grace Mugabe, pamoja na kubaki
na mali zake zote.Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na timu ya majadilliano
kimeliambia shirika la utangazaji la CNN kwamba Mugabe ameshaandaa barua
ya kujiuzulu.
Chanzo hicho
kimeeleza kwamba majenerali wa jeshi la nchi hiyo wameridhia matakwa
hayo. CNN limeambiwa kwamba chini ya makubaliano hayo, Mugabe na Grace
hawatashtakiwa.
Pia, viongozi
wawili waandamizi wa serikali ya Mugabe wameliambia shirika la habari la
Reuters Jumapili kwamba Mugabe alikuwa amekubali kujiuzulu lakini hawakuwa
wanajua yaliyomo katika mkataba wa kuondoka kwake.
“Ili ionekane
amejiuzulu rasmi, utaratibu ni kwamba barua lazima iandikwe kwenda kwa Spika wa
Bunge”, Chanzo kingine kimeongeza.
Mugabe ambaye
anakabiliwa na shinikizo la kuachia wadhifa wake jana aliwashangaza watu kwa
kushindwa kutangaza kujiuzulukinyume na matarajio ya wengi alipokuwa
akilihutubia Taifa kwa njia ya Televisheni.
Aidha chama
chake cha Zanu -PF kilikuwa kimempa kimempa muda hadi kufikia mchana wa leo awe
ameng’atua na kama asipofanya hivyo atashtakiwa bungeni.
Mwishoni mwa wiki iliyopita,
maelfu ya wananchi wa Zimbabwe wakiongozwa na jeshi waliaandamana kwa ajili
yakumshinikiza ajiuzulu.
Comments