Katibu wa wizara ya fedha na mipango Dotto James pamoja Mkuu wa ushirikiano wa maendeleo, ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting wakisaini mikataba
Na Mwandishi wetu Dar es salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea msaada wa jumla ya shil. bill.435.79 kutoka kwa serikali ya Sweden kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
Hayo yamebainishwa leo na Katibu wa wizara ya fedha na mipango Dotto James wakati wakisaini mikataba mitatu ya makubaliano ya msaada wa kibajeti ukilenga kuimarisha maendeleo mbalimbali nchini ikiwemo miundombinu na kuboresha sekta ya elimu.
James amesema mikataba hiyo itasaidia utekelezaji wa bajeti ya kila mwaka lakini pia kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake na ukilenga maeneo ya kuboresha uhalisia wa bajeti ili kuweza kutimiza majukumu mbalimbali yaliyokusudiwa kwenye bajeti ya serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa ushirikiano wa maendeleo, ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting watahakikisha wanaendeleza ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo kuboresha sekta ya elimu.
Comments