Waam,uzi wa mchezo wa Azam FC vs Mibwa Sugar wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi
Mwamuzi
wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana aliyechezesha mechi kati ya Azam FC
dhidi ya Mtibwa Sugar ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi
watakaoendelea kuchezesha mashindano ya Mapinduzi Cup kufuatia kulikataa
bao la Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumapili January
3, 2015.
Mwamuzi
huyo alilikataa bao halali lililofungwa na Kichuya wa Mtibwa Sugar
kipindi cha pili cha mchezo huo ambalo lingeipa ushindi timu ya Mtibwa
Sugar kwenye mcheo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kukataliwa
kwa bao hilo kulizua tafrani kati ya waamuzi waliochezesha mchezo huo
dhidi ya wachezaji wa Mtibwa na bechi zima la ufundi hali iliyolazimu
jeshi la polisi kuwatoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi
mkali.
Katibu wa
kamati ya ZFA Hashim Salum Hashim amemwandikia barua ya kumwondoa
kwenye mashindano ya Mapinduzi mwamuzi huyo kutokana na kutokuwa makini
kwenye mchezo kati ya Azam FC vs Mtibwa Sugar.
Hapa chini kuna barua kutoka kwa katibu wa ZFA ya kumwondoa kwenye mashindano mwamuzi Dalila Jaffar Mtwana. Shaffihdauda.com(P.T)
Comments