Nyota wa zamani wa Uingereza Ashley Cole amethibitisha kujiunga na LA Galaxy ya Major League Soccer nchini Marekani.
Baada ya kushindwa kufanya vizuri na Roma ya Italia, Cole ataungana
na akina Robbie Keane na Steven Gerrard kwenye klabu ya Los Angeles.
Cole, ambaye alizichezea Arsenal na Chelsea kabla ya kutimkia Rome,
alicheza mechi 11 katika miezi 18 klabuni hapo, na hakuwahi kucheza hata
dakika moja msimu huu.
HISTORIA YA SOKA YA ASHLEY COLE
Arsenal 228 games (9 magoli)
Crystal Palace (mkopo) 14 (1)
Chelsea 339 (7)
Roma 16 (0)
England 107 (0)
Heshima kubwa:
Premier League: 2002, 2004, 2010
FA Cup: 2002, 2003, 2005, 2007, 2009, 2010, 2012
Champions League 2012
Europa League: 2013
Comments