Yaya Toure ametoa mashambulizi ya hasira kwa kuliita Shirikisho la
soka Afrika (CAF) kwamba halina maadili na huruma baada kukosa Tuzo ya
Mchezaji bora wa Mwaka.
Kiungo huyo wa Manchester City, ambaye ameshinda tuzo hiyo mara nne,
alishindwa na mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.
Aubameyang, aliyezaliwa nchini Ufaransa lakini ni mshambuliaji wa
Gabon, amefunga magoli 24 katika michezo 23 kwenye msimu huu na anawinda
Ligi Kuu.
Lakini Toure hakumumunya maneno yake, akitoa malalamiko kwa kile
kinachoonekana kama shirikisho hilo halijaona ushindi wa Ivory Coast
kwenye Kombe la Mataifa Afrika mwezi Februari.
“Nimekatishwa tamaa sana. Ni huzuni kuona Afrika inafanya namna hii,
kwamba hawafikirii mafanikio ya Afrika ni muhimu,” aliiambia redio ya
Ufaransa ya RFI.
“Nafikiri hichi ndicho kinacholeta aibu Afrika, kwa sababu kufanya
hivi si uadilifu. Lakini tunaweza kufanya nini? Sisi Waafrika,
hatuonyeshi kwamba Afrika ni muhimu machoni mwetu. Tunapendelea nje
zaidi kuliko nyumbani kwetu. Inatia huruma.
Comments