YANGA imevunja ratiba yao ya kucheza na Coasta Union katika mchezo wa
Ligi baada ya kutangaza kikosi chao kwenda Afrika Kusini katika
mashindano mafupi.
Mkuu wa Idara na Mawasiliano ya Yanga Jerry Muro amesema kikosi chao
kinatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa ya wiki hii tayari kwa mashindano
hayo ambayo hata hivyo hawakuyaweka wazi.
Muro amesema safari hiyo inataka kutumiwa na kikosi chao katika
kujiweka sawa kabla ya kuanza mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika
ambayo timu hiyo itafungua dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius kati
ya Februari 12-14.
“Barua rasmi itapelekwa TFF na Katibu wetu Baraka Deusdedit kesho
kuweza kuwajulisha kwamba tunalazimika kwenda huko baada ya uongozi wetu
kukubali mualiko huo ambao ulifika muda tu lakini kuna mambo tulitaka
yawekwe sawa,” amesema Muro.
“Kwasasa timu tutakazocheza nazo tutaziweka wazi baada ya kupata
ratiba lakini pia ikumbukwe kwamba tunashiriki Ligi ya Mabingwa sasa
tutatumia nafasi hiyo kama sehemu ya maandalizi.”
Comments