Nyota wa Barcelona wameonekana kutawala katika kikosi cha Timu ya
Mwaka ya UEFA huku kukiwa hakuna hata mchezaji mmoja wa Ligi Kuu
kushiriki katika kikosi hiko.
UEFA ilitangaza kikosi hiko siku ya Ijumaa asubuhi baada kupigiwa kura na watumiaji wa mtandao wao.
Washambuliaji wawili wa Barcelona Lionel Messi na Neymar ndio
wanaounda safu ya mbele ya 4-3-3 wakishirikiana na mfungaji magoli wa
Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Lionel Messi alijizolea kura 448,445 kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa UEFA.
Katika kikosi hiko wamo nyota wengine wa Barca kama Dani Alves, Gerard Pique na Andres Iniesta.
Wengine kutoka ligi nyingine ni Manuel Neuer, David Alaba na Paul Pogba.
Comments