Meneja wa Chakula na Vinywaji wa Shirika la Ndege la Etihad.
Etihad Business Studio.
Shirika
la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la Mwaka wakati wa
tuzo za Business Travel 2016. Hafla hii ilifanyika jana usiku katika
hoteli ya Grosvenor House iliyopo Jijini London. Tuzo hizi zinatambua
makampuni na watu binafsi waliopata mafanikio katika sekta ya biashara
ya usafiri na hivyo kuwafanya wastahili kuwania tuzo hizo.
Tuzo hizi
zinazoandaliwa na jarida la Uingereza la Buying Business Travel, huwa
na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura kubaini
washindi. Hii ni mara ya kwanza kwa Etihad kushinda tuzo hiyo, hii ikija
siku chache tu baada ya shirika la ndege la Etihad kupokea “Tuzo ya
Uvumbuzi katika Usafiri” kutoka tuzo za jarida la Globe Travel katika
hafla nyingine iliyofanyika wiki iliyopita London.
James
Harrison, Meneja Mkuu wa shirika la Etihad Uingereza, alisema: “Tuzo hii
ni ishara ya kutambulika kwa mchango wa Etihad katika sekta ya usafiri
wa anga nchini Uingereza. Tunajisikia fahari kubwa sana kutambuliwa
katika jukwaa kubwa hivi.”
“Uingereza
ni soko muhimu kwa shirika hili na mwaka huu umekuwa na mafanikio
makubwa kwetu kwani tunasherekea miaka kumi tangu tuanze kutoa huduma
zetu kati ya jiji la Manchester na Abu Dhabi. Tunategemea kuzindua
huduma ya tatu ya kila siku kutoka uwanja wa ndege Heathrow, jijini
London, kupitia ndege aina ya A380 ambayo pia ina huduma ya vyumba ya
“Makazi”. Zaidi tunalenga kutoa huduma iliyorahisishwa na
inayowaunganisha wageni wetu.”
Shirika
la Etihad liliibuka kidedea kutokana na huduma zao za hali ya juu,
zikiwemo bidhaa (na vyumba) zilizoingia hivi karibuni sokoni na kuleta
mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga. Hii ikiwa pamoja na kutumia
ndege aina ya Airbus A380 na Boeing 787 Dreamliners, bila kusahau vyumba
ambavyo vilishakuwa vikitumika na Airbus A330/A340 na Boeing 777.
Mapinduzi
haya yametokana na programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa
katika Kituo cha Uvumbuzi kilichopo Abu Dhabi na kuongozwa na timu ya
ubunifu ya Etihad. Shirika la Etihad linapenda kutoa huduma yenye
viwango sawa na hoteli kubwa na sehemu nyingine za kitalii kubwa
duniani. Etihad wameajiri wafanyakazi wenye ufundi na uzoefu mkubwa
haswa katika safari ndefu kwa mfano wahudumu wakuu walipo katika
“Makazi” ya ndege ya A380 kwenda London, Wapishi Wa daraja la Kwanza,
meneja wa vyakula na Vinywaji katika “daraja la biashara” na wahudumu wa
kutunza watoto wakati wa safari. Wahudumu hawa wamehitimu chuo cha
kulea na kutunza watoto Norland huko Uingereza.
Pia
shirika la ndege la Etihad lina sehemu ya mapumziko katika viwanja vya
ndege wa London Heathrow, Manchester, Frankfurt, Dublin, Paris, Sydney,
Washington, D.C. na New York wakati uwanja wa ndege wa Abu Dhabi una
sehemu za mapumziko na mapokezi.
Hivi sasa
safari za shirika hili zinafika sita kila siku kwenda Uingereza, zikiwa
na huduma za moja kwa moja kufika jijini London kupitia uwanja wa ndege
wa Heathrow, jijini Manchester na jijini Edinburgh zilizozinduliwa Juni
8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow Jijini London ulipata nafasi
ya kuwa kituo cha kwanza kwa ajili ya kuzindua huduma ya ndege za jamii
aina ya Airbus A380, ikiwemo huduma ya “Makazi”- ikiwa na vyumba vya
kipekee duniani kuwekwa kwenye ndege ya kibiashara yenye ukubwa wa
vyumba vitatu huku ndege hii pia ikiwa na vyumba 6 vya “daraja la
kwanza”, 70 vya “daraja la biashara” na 415 vya “daraja la uchumi”.
Comments