Kuna taarifa za wasiwasi kwamba huenda Mbwana Samatta asijiunge na
klabu Genk ya Ubelgiji kwasababu bado ana mkataba na klabu ya TP Mazembe
na bosi wa klabu hiyo Moise Katumbi hayuko tayari kuona nyota huyo
kipenzi cha wana-Lubumbashi anaondoka kunako klabu ya Mazembe.
Mtandao huu ukabisha hodi kwa manager wa Mbwana Samatta Mr. Jamal
Kisongo ambaye yeye ndiye anayesimamia kila kitu kuhusu masuala ya
usajilki na mikataba ya mchezaji huyo.
Kisongo amefafanua kila kitu kuhusu mkataba wa Samatta uliobaki
kuendelea kuitumikia TP Mazembe pamoja na taratibu zilizofikiwa ili
kuhakikisha Samatta anakwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Hii
hapa story nzima ya Kisongi akifunguka juu ya mustakabali mzima wa
Samatta kuhusu kutimkia Ulaya kwenye klabu ya Genk.
Suala la Mbwana kucheza soka Ulaya limefikia tamati
kwasababu kitu kikubwa zadi tayari ameshasaini mkataba na klabu ya Genk
mkataba wa miaka miwili lakini akiwa na nafasi akitaka kuongeza miaka
miwili mingine anaweza kufanya hivyo. Kwahiyo watanzania wawe na amani
kwasababu Mbwana ni mchezaji halali wa Genk.
Sasa hii sintofahamu nyingine ya utaratibu wa uhamisho
ndiyo unaleta shida, lakini Mbwana amebakiza mkataba wa miezi minne na
kwa mujibu wa kanuni za FIFA mchezaji anapobakiza mkataba wa miezi sita
na chini ya hapo ana haki ya kujadili mkataba mpya na klabu yoyote au
kutaka kujua hatma yake ili mkataba wake unapokwisha asibaki bila timu
kwasababu FIFA inataka wakati wote mchezaji awe na timu.
Ukizingatia mwezi April ukimalizika hakuna dirisha la
usajili, usajili upo mwezi January na mwezi July, tafsiri yake ni kwamba
tulichokifanya kwa Mbwana ni kuhakikisha mwezi Janury anaitumikia Genk
lakini ukisema asubiri hadi mwezi wa saba maana yake kunakipindi atabaki
akiwa mchezaji ambaye hana timu kwasababu mkataba wake na Mazembe
unamalizika mwezi April.
Kwahiyo Mbwana kubaki bila timu kutatoa nafasi ya
kumshawishi aendelee kubaki TP Mazembe lakini watanzania wengi wanataka
kumuona Samatta akiingia kucheza Ulaya kwasababu ana kila aina ya sifa
zaidi ya wachezaji wengi wa Afrika Magharibi, Kaskazini na Kusini mwa
Afrika.
Huu utata uliopo unatokana na madai ya kipesa (ada ya
uhamisho) TP Mazembe wao wanataka walipwe Euro milioni 2.5 ambayo pesa
hii ukizingatia miezi minne au mitatu itakayobaki baada ya mwezi Janury
ni pesa nyingi mno ukilinganisha na mkataba halisi wa Mbwana uliobaki.
Kwahiyo Genk wakasema hapana, TP Mazembe wakatoa nafasi kwa Genk waseme
wao wako tayari kutoa kiasi gani cha pesa.
Genk wakatoa offer ya Euro 350,000 ambayo Moise Katumbi
akaona ni pesa ndogo mno akarudisha na kuwaambia waongeze offer, Genk
wakapeleka offer nyingine ya Euro 550,000 ambayo pia ilikataliwa na
Katumbi ambaye alisema anataka Euro 750,000.
Mimi nikalazimika kwenda Lubumbashi kuzungumza na Katumbi
ili amwachie Mbwana, kwasababu wakati Mbwana anasaini mkataba na TP
Mazembe kuna vitu ambavyo tuliafikiana. Mimi kama manager wake kwa faida
ya mtoto (wakati huo Mbwana alikuwa bado mtoto) tulikubaliana ndani ya
miaka miwili au mitatu Mbwana aondoke.
Lakini imefikia kipindi offer nyingi zilizokuwa zinaletwa
kwake yeye alikuwa nazitia kapuni, kwahiyo tulizungumza na yeye akatoa
masharti kwamba Mbwana aongeze mkataba wake kwa miaka mitatu ambao
utamruhusu kuondoka kitu ambacho kwangu kilikuwa ni kigumu.
Tulimwita mwanasheria wetu tukakaa na Frederic Kitengie
tukakaa vikao kwa siku mbili lakini havikuzaa matunda kwasababu wao
walikuwa wanalazimisha Mbwana asaini mkataba kwao kwa madai ya kumpa
thamani.
Sisi pia tukatoa masharti yetu. Mwanasheria wetu akasema,
Mbwana anaweza kusaini mkataba ikiwa kutakuwa na kifungu kinachosema ni
lazima auzwe mwezi January na siyo kutolewa kwa mkopo kwasababu Katumbi
huwa hauzi wachezaji kwenda Ulaya badala yake huwa anawatoa kwa mkopo.
Na wao pia wakakataa sharti hilo.
Genk nao wakachua hatua, wameamua kulipeleka suala hili
FIFA. Baada ya kutua FIFA, Katumbi alipigiwa simu na watu wa Genk
hakupokea lakini baaye aliwapigia simu wakaweza kujadili lakini suala
hili bado limekwama. Kwahiyo cha msingi tunataka kuwaambia watanzania
wawe na amani Mbwana ni mchezaji halali wa Genk.
Suala lililopo na tunachoshindana ni kwamba Mbwana
aondoke January au majira ya joto, sisi tunachotaka aondoke majira haya
ya baridi (mwezi Janury).Inatoka http://shaffihdauda.co.tz
Comments