Alikaribisha mtoto wa tatu wa kiume duniani wikiendi hii.
Siku ya Jumatatu, Wayne Rooney alikuwa na furaha kama baba alipotuma
picha nzuri Instagram ya mwanae mwingine, Kit, akiwa na umri wa dakika
kadhaa.
“Nakutana na Kit kwa mara ya kwanza. Muda wa kwenda nyumbani sasa,” mchezaji huyo aliandika katika picha hiyo.
Rooney, 30, na mkewe Coleen walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kiume – waliompa jina la Kit Joseph Roone – siku ya Jumapili.
Awali Coleen, 29, aliwahi kuzungumza kuwa anatamani kupata mtoto wa kike.
Comments