Liverpool wanataka kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex
Teixeira mwenye asili ya kibrazil na kama dili hilo litafanikiwa huo
utakuwa ni usajili mkubwa wa kwanza kufanywa na kocha Jurgen Klopp tangu
awe manager wa kikosi cha Liverpool.
Wekundu hao wako tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 24.5 kwa ajili
ya kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 26. Klabu ya nyota huyo
ambaye pia anahusishwa na Chelsea imeweka dau la pauni milioni 39 kwa
klabu inayotaka kumsajili mshambuliaji wao.
Klopp anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kuwa
washambuliaji wake wengi ni majeruhi kwa sasa, Danny Ings, Divock Origi
pamoja na Daniel Sturridge wote wanauguza majeraha.
Usajili wa pauni milioni 32.5 kumnasa Christian Benteke umeshindwa
kuzaa matunda yaliyotarajiwa baada ya timu hiyo kujikuta ikufunga mabao
25 katika mechi 22 za ligi kuu England hadi sasa.
Teixeira ameshatupia kambani jumla ya magoli 22 kwenye mechi 15 za
ligi na magoli mengine 10 kwenye michuano ya klabu bingwa msimu huu.
Nyota huyo alianzia soka lake kwenye klabu ya Vasco da Gama ya Brazil kabla ya kuhamia Shakhtar mwaka 2010.
Klopp amemsajili kwa mkopo beki Steven Caulker wa QPR na amekamilisha
dili la kinda mwenye miaka 19 Marko Grujic kwa pauni milioni 5.1 ambaye
ameachwa kwa mkopo kwenye klabu ya Belgrade hadi majira ya joto.
Usajili wa Teixeira utakuwa ni usajili wa kwanza mkubwa kwa Klopp
kwenye soko la usajili na mshambuliaji huyo atakuwa ni mbrazil wa nne
kwenye kikosi cha Liverpool akiwa ametanguliwa na Lucas Leiva, Roberto
Firmino na Philippe Coutinho.
Comments