NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mazingira na Muungano) Luhaga Mpina
amempatia saa 48 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kujieleza
sababu za Jiji la Mwanza kuwa chafu.
Mpina alisema hayo jana jijini hapa wakati akieleza mambo aliyoyabaini wakati wa ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza.
Alisema licha ya serikali kutangaza suala la usafi kuwa ni hoja ya kitaifa, Jiji la Mwanza linatisha kwa uchafu wa mazingira.
Mpina ambaye alianza ziara jana kukagua maeneo mbalimbali ya jiji,
alisema uchafu wa jiji kwa kiwango kikubwa unachangiwa na baadhi ya
watendaji wa Serikali na wataalamu, kutowajibika vyema.
“ Ni sehemu ndogo tu ya uchafu wa jiji la Mwanza unaochangiwa na
wananchi, kutokana na hali hii nilivyoiona ninampatia Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Magesa Mulongo masaa 48 ajieleze ni kwanini jiji la Mwanza ni
chafu ilihali lina watendaji wa kutosha na wataalamu”, alisema.
Alisema Januari 30 mwaka huu atarudi jijini Mwanza, kushiriki usafi na
wananchi kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya
Tano.chanzo kimoja kimeripoti.
Comments