Mwanasaikolojia
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa
Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na Taasisi ya Manjano foundation
yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo
ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch
Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya
Manjano Foundation yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti
Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo
yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake
hao kujitambua wao ni nani wana nafasi gani kwenye jamii
inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila
wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa kwenye Mafunzo hayo.
Pia
amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia
FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi
wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi
humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma
yake yaani "Smart You & Environment."(P.T)
Semina
hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na
pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.
Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa
MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano Foundation kupitia vipodozi vya
LuvTouch Manjano.
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza
waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na
Taasisi ya Manjano Foundation.
Washiriki
wa mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano Foundation
kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi
wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi
sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.
Comments