Pep Guardiola anakuja Ligi Kuu baada ya kuthibitisha nia yake ya
kufanya kazi nchini Uingereza wakati atakapoondoka Bayern Munich katika
majira ya joto.
Manchester City ndio wanaotazamiwa kumpokea kocha wa zamani wa
Barcelona, 44, japokuwa inafahamika kwamba hajasaini mkataba wowote
Etihad.
Na City inaweza kupata ushindani kutoka Chelsea, Manchester United na
hata Arsenal katika kumnasa mmoja wa makocha wenye mafanikio katika
soka duniani.
Guardiola alifanya kazi na mkurugenzi mtendaji wa City Ferran Soriano
na kiongozi wa soka Txiki Begirotain Barcelona, ambapo alishinda Ligi
ya Mabingwa mara mbili, mataji matatu ya La Liga, makombe mawili ya
Hispania na Makombe mawili ya Dunia.
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu atangaze mwezi
uliopita kwamba ataondoka Bayern Munich baada ya kuitumikia kwa miaka
mitatu, Guardiola alisema: “Sababu iliyonifanya nisiongeze mkataba ni
rahisi; Nataka kuwa kocha katika Ligi Kuu.”
“Nina ofa kadhaa kutoka Uingereza, lakini sijaamua kujitoa kwanza.
Nikishapata klabu mpya, hiyo klabu italitangaza hilo. Kwa sasa hakuna
kilichofanyika.”
“Kama ningekuwa na miaka 60 au 65 ningebaki lakini nafikiri bado ni
mdogo. Nahitaji changamoto mpya. Ilikuwa ni ndoto, bado ni ndoto.
Naishukuru Bayern Munich kwa fursa yake kubwa. Nitafanya vizuri siku za
mwisho.”
Comments