Kundi la IS hutekeleza sheria kali za Kiislamu
Mpiganaji
wa kundi la Islamic State nchini Syria amemuua mamake hadharani kwa
sababu alimwambia ahame kundi hilo, wanaharakati wanasema.
Ali Saqr, 21, alimuua mamake, Lena al-Qasem, 45, nje ya afisi ya posta mjini Raqqa, Syria, watu walioshuhudia wanasema.
Mji wa Raqqa umekuwa ukihudumu kama mji mkuu wa IS tangu wapiganaji hao kutekwa mji huo Agosti 2013.
Kundi
hilo huwa halivumilii watu wanaopinga msimamo wake na kutoa adhabu kali
kwa wanaopinga kundi hilo, na mara nyingi adhabu hutekelezwa hadharani.
Maafisa
wa Shirika la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) lenye makao
yake Uingereza na kundi la wanaharakati wa Raqqa is Being Slaughtered
Silently (Raqqa Inachinjwa Kimy akimya) wamethibitisha kisa hicho.
Lena
al-Qasem alikuwa amemwambia mwanawe kwamba muungano unaoongozwa na
Marekani ungeangamiza kundi hilo, na akajaribu kumshawishi ahame mji huo
pamoja naye.
Mwanawe alijulisha wenzake katika IS, na agizo likatolewa auawe.
Ali Saqr anadaiwa kumpiga risasi mamake nye ya afisi ya posta mbele ya mamia ya watu.
Kundi la IS hutekeleza sheria kali za Kiislamu, zenye kuegemea madhehebu ya Kisuni.
Kundi hilo limedhibiti maeneo ya Iraq na Syria tangu 2014.BBC
Comments