Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF litafanyika Februari 23 mwaka kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Jumla ya Tuzo 30 za Filamu zinatarajiwa kutolewa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF litatalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Februari 23 mwaka huu.
filamu zilizotajwa kuingia katika duru ya pili kwa upande wa filamu ndefu za kiswahili ambazo zilikuwa 141 zilizoingia duru ya pili ni 28, filamu fupi ni 73 zilizoingia 11, tamthili 20 zilizopita ni 7, makala zilizopita 3 huku kila kipengele kikitofautiana idadi ya Filamu kutokana na ushindani uliokuwepo ambapo vigezo na masharti yakizingatiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati akitangazafilamu zilizopita katika mchujo wa kwanza Mratibu wa Tamasha hilo Sophia amezitaja filamu zilizoingia katika duru ya pili kwa upande wa filamu ndefu za kiswahiliambazo zilikuwa 141 zilizoingia duru ya pili ni 28, filamu fupi ni 73 zilizoingia 11, tamthili 20 zilizopita ni 7, makala zilizopita 3 huku kila kipengele kikitofautiana idadi ya Filamu kutokana na ushindani uliokuwepo ambapo vigezo na masharti yakizingatiwa.
Amesema tuzo za SZIFF zimegawanyika katika makundi mawili zikiwemo za Swahili Panorama ikijumuisha filamu zote zilizosajiliwa moja kwa moja katika tuzo hizo huku kundi la pili likijumuisha World Cinema zilizosajiliwa zikitumia lugha ya kigeni zikiwa na tafsiri ya Kiingereza hususan kwa zile ambazo hazikuandaliwa kwa lugha hiyo.
"Kipengele kipya cha World Cinema ambacho kimesajili Filamu kutoka nchi zaidi ya 15 toka maeneo mbalimbali ulimwenguni imekuwa ni nafasi muhimu ya kupima filamu za kitanzani na za kiafrika katika kuongeza ubunifu na weledi katika kuandaa kazi za filamu zitakazoweza kufanya vizuri kimataifa,"Amesema.
Naye Mkurugenzi Uendeshaji vipindi wa Televisheni ya Azam, Yahaya Mohamed amesema kwa takribani mwezi mmoja na nusu Chaneli ya Sinema Zetu ilionyesha filamu zote zilizopita duru la kwanza ambapo 237 zilionyeshwa zikijumuishwa filamu ndefu, fupi, tamthiliya pamoja na makala.
Ameabinisha kuwa tuzo za SZIFF zimegawanyika katiika makundi mawili zikiwemo za Swahili Panorama ikijumuisha filamu zote zilizosajiliwa moja kwa moja katika tuzo hizo huku kundi la pili likijumuisha World Cinema zilizosajiliwa zikitumia lugha ya kigeni zikiwa na tafsiri ya Kiingereza hususan kwa zile ambazo hazikuandaliwa kwa lugha hiyo.
“ Tamasha la SZIFF leo linatangaza filamu zilizopita katika mchujo wa mwanzo ili kuwania tuzo za sinema zetu kwa mwaka huu,” amesema Mohamed.
“ Tamasha la SZIFF leo linatangaza filamu zilizopita katika mchujo wa mwanzo ili kuwania tuzo za sinema zetu kwa mwaka huu,” amesema Mohamed.
Amesisitiza kuwa katika kuhakikisha tamasha hilo linakuwa karibu na watazamaji na kupanua wigo wa ushindani miongoni mwa wasanii na wadau wa sanaa Afrika wameongeza vipengele viwili vipya kikiwemo kipengele cha Tamthiliya na World Cinema.
Amefafanua kuwa katika kipengele cha Tamthiliya tuzo zitakazoshindaniwa ni Tuzo ya Tamthiliya bora, Muongozaji bora, Mwandishi bora, Mhariri bora wa picha jongevu huku za world cinema zitakuwa ni mtunzi bora wa muziki asili pamoja na mpiga picha bora, Muigizaji bora wa kike na kiume na filamu bora.
Amesema washindi watapata zawadi kati ya Sh milioni moja hadi milioni 5 kulingana na ukubwa wa tuzo pamoja na cheti cha tuzo hizo huku akibainisha upatikanaji wa washindi wa kila kipengele watakaowania tuzo 30 umegawanyika katika sehemu mbili wakiwemo washiriki waliochaguliwa na Jopo la Majaji kwa kuzingatia vigezo na mashati na kwamba sehemu ya pili ni washiriki waliochaguliwa na watazamaji kupitia tovuti na ujumbe wa meseji.
Miongoni mwa filamu zilizoingia duru la pili zimetajwa kuwa ni Iyango, Petu na Guru, Siyabonga, Kiumeni, Mama Afrika, Dema, Safari pamoja na T-Junction.
Nyingine upande wa filamu za vichekesho ni Kazoa ndani ya Imani, Mama Mwali, Mchumia pamoja na Mwali wa Kijiji.
Ambapo filamu zingine zilizoingia duru la pili zitaanza kuonyeshwa leo Saa 10 jioni katika Chaneli ya Sinema Zetu.
Naye Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Profesa Martin Mhando amesema upatikanaji wa washiriki katika kila kipengele umezingatia vigezo vingi na kwamba filamu zlizoshinda duru la pili ni zile zenye ubora wa hali ya juu.
Pia ameongeza kuwa mwaka uliopita Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete alikuwa mgeni wa heshima katika hafla ya tamasha hilo lililovutia wengi na kwamba kwa mwaka huu mgeni rasmi bado hajawekwa wazi.
Comments