KAMPUNI ya mawasiliano ya simu halotel imekuja na huduma 2 ya Royal bundle
na Tomato bundle ambazo zitawawezesha wateja kupata huduma zisizo na kikomo
kwa kupiga simu ndani na kimataifa pamoja na kutumia intanenti bila kikomo.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi leo jijini Dar es salaam,mkurugenzi mkuu wa
halotel Tanzania Nguyen Van Trung alisema kuwa huduma hizo zitawapa ubora na
unafuu wateja wao kila kona ya nchi.
"Ninayo furaha kubwa kuwatangazia ujio wa huduma hii kabambe itakayoleta mapinduzi
makubwa nchini Royal bundle imekuja kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatani
kutumia huduma zetu bila kupata bugudha zikiwemo salio kuisha au intaneti kukata,"
alisema Nguyen
pICHANI Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za Mkononi Halotel Bw. Nguyen Van Trung akimmiminia mvinyo Diva mtangazaji wa Clouds kulia ni DJ Makay kutoka East Africa Radio pamoja na wasanii mbalimbali ambao ni mabalozi wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za kupiga simu ya Royal Bando na Tomato Bando zilizozinduliwa leo .
Nguyen alisema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shughuli za kiuchumi
hivyo tusingependa halotel kuwa kikwazo katika kufanikisha hilo.
Hata hivyo Kampuni yetu inawatangazia watanzania wote kuwa shilingi 10000 tu unaweza
kupiga simu za ndani na kimataifa kama vile kwenye nchi za India,China,Canada na Marekani
bila ya kikomo,kutumia intaneti na SMS bila kikomo.
"Kama nilivyosema awali,huduma hii inawalenga wateja ambao hawapendi bugudha katika
mawasiliano,pia na fursa kwa wateja ambao wamekwisha fanyiwa usajili na halotel ambapo
kwa wateja wapya hao wataunganishwa moja kwa moja kwa gharama niliyoitaja awali bila
kuweka salio," alisema Van Trung
Alisema utapata faida nyingi endapo utajiunga na hudama hii ambapo shilingi 10000 kwa
mwezi mteja atajipatia muda wa maongezi wa dakika 520 kupiga simu mitandao yote
kifurushi cha intaneti yenye kasi cha GB 2 pamoja na kuwezeshwa SMS 500.
Mkurugenzi huyo alitumia fursa kuielezea huduma nyingine ya Tomato bundle ambayo
ni maalumu kwa wateja wa halotel ambayo itawawezesha kupiga simu bure kwenda namba
yeyote ya halotel kwa dakika 5 za mwanzo kwa kila simu na kupata salio la shilingi
4000 bure.
"Kwa upande mwingine halotel inawaleteeni huduma ya Tomato bundle ili wateja waweze
kufurahia hivyo tunawataka wawe na laini ya halotel ya tomato itakayo patikana kwa
kiasi cha shilingi 8000 hiyo itamwezesha mteja kupiga simu kwa namba ya halotel bure
kwa dakika za mwanzo.
Comments