Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel imewakabidhi zawadi za Simu za Smartphone ICE2 washindi wa Jumatano ya wiki iliyopita wa Droo ya Wiki ya Tumia Eazy Pesa Ushinde.
Akikabidhi zawadi hizo kwa washindi wa droo hiyo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa amesema washindi 30 wa wiki wamekabidhiwa zawadi hizo ambapo kati yao watano wamepewa jijini humo huku 25 waliobaki wanatoka Visiwa vya Unguja na Pemba.
“ Tulifanya droo ya Tumia Eazypesa Ushinde Jumatano iliyopita washindi 30 wanakabidhiwa zawadi ya Simu ya Smartphone ICE2 watano wanakabidhiwa hapa mmoja wao anaishi Dar waliobaki Unguja na Pemba,” amesema Rukia.
Amebainisha kuwa washindi wa droo ya mwezi ya Tumia Eazypesa na Ushinde watakabidhiwa fedha taslimu ambapo mshindi wa kwanza atapata Sh milioni moja, wa pili Sh 500,000, wa tatu Sh 300,00 huku mshindi wa nne hadi wa 10 kila mmoja atakabidhiwa Sh 200,000.
Amewataja miongoni mwa washindi hao ni Mohamed Kapoma, Suleiman Ally Suleiman mkazi wa Ukonga, Swibawahi Sheikh na Jabir Abdallah.
Mshindi wa droo hiyo, Suleiman amesema alipopigiwa simu kuambiwa ameshinda hakuamini lakini baadaye aliamini hivyo aliwataka wananchi kujiunga na mtandao wa Zantel kupata zawadi na huduma bora.
Naye mshindi, Swibawahi amesema alipigiwa simu akiwa nyumbani na kwamba amefurahi kupata zawadi hiyo na kwamba amewaomba wananchi wajiunge ili washinde.
Comments