Leo kuanzia saa mbili asubuhi makamanda na wanachama wa CHADEMA na
wananchi wasio na vyama vya siasa walikusanyika katika mtaa wa Nyasura
iliyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kwa ajili ya kuanza
maandamano ya kupinga Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake.
Wananchi waliojitokeza walikuwa karibu 1,200 na ilipofika saa tano
kamili maandano yalianza kuelekea stendi ya zamani ambapo ilitalakiwa
ufanyike mkutano mkubwa, polisi walikuja na kuanza kurusha mabomu ya
machozi na kwa kuwa wananchi walikuwa wamejizatiti, mabomu ya machozi ni
kama hayakufua dafu ndipo risasi za moto zilianza kutumika.
Mpaka sasa wameshakamatwa viongozi sita wa Chadema.
Wananchi bado wanaendelea kujikusanya na kutiana hamasa!
Shuhuda mmoja alisema ameona makundi makubwa ya watu sasa yanatoka
kwenye nyumba zao na wameanza kujikusanya wakiwa na lengo la kuendelea
na maandamano!
Habari zaidi inafuatia…
Chanzo: JamiiForums.
Comments