Mashambulizi nchini Ukraine
Milipuko mikali imesikika katika mji wa Bandari wa Mariupol mashariki mwa Ukraine.
Waandishi walioshuhudia makombora hayo
wanasema kuwa kizuizi muhimu cha serikali kiliharibiwa na mashambulizi
makali kutoka kwa wapiganaji wanaounga mkono Urusi.
Mji wa Mariupol unaonekana na
wapiganaji wanaounga mkono Urusi kama muhimu katika barabara inayoelekea
Crimea mbali na kuwa kitega uchumi cha eneo la Donbas iwapo litakuwa
huru.
Mwandishi wa BBC katika mji huo
amesema kuwa haijulikani iwapo mashambulizi hayo ni ya mda ama ni mwisho
wa makubaliano ya kusitisha vita yalioafikiwa siku ya ijumaa.Awali viongozi wa Urusi na Ukraine walisema kuwa wameridhika kuwa makubaliano hayo yanaafikiwa.
Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Ukraine Petro Porishenko walizungumza kuhusu mwafaka huo kupitia njia ya simu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa makombora yaliyalazimu malori ya misaada yaliokuwa yakielekea katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Luhansk kurudi.
CHANZO: BBC SWAHILI
Comments