Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller wakati wa mkutano wa kuzungumzia masuala ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya barani Afrika.(P.T)
Comments