Amissi Tambwe mshambuliaji wa Simba SC amejipanga vyema
kuhakikisha anaendelea na moto wake wa ufungaji wa mabao mengi katika
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu.
Tambwe aliibuka mfungaji bora wa kombe la Kagame mwaka jana na
vilevile mfungaji bora katika ligi kuu Tanzania bara kwa kufunga mabao
19 katika michezo 23 aliyocheza katika timu yake ya Simba .
Akifanya mazungumzo na vyombo vya habari jana,Tambwe anaamini usajili
uliofanywa na Simba kwa kuweza kumrudisha Okwi katika timu yao ni mzuri
sana kwa timu na hasa kwake yeye kwani atacheza sambamba na yeye na
kuweza kumtengenezea nafasi nyingi za kufunga mabao mengi msimu huu.
Chanzo : kandanda.galacha.com
Comments