Akiongea na Times Fm, Witness ameeleza kuwa alikuwa anatarajia
mapacha na alikuwa katika hatua za mwisho lakini ghafla ikatokea hali
hiyo ambayo hadi sasa inafanyiwa uchunguzi na madaktari kubaini chanzo.
“Kuna mambo ambayo niliambiwa kwamba endapo ningekuwa sina mazoezi au
ningekuwa siko strong ina maanisha kwamba na mimi mwenyewe ningekuwa
hatarini.” Amesema Witness.
Ameeleza kuwa hali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita lakini yeye na
mchumba wake Ochu waliamua kukaa kimya kwa muda hadi leo walipoamua
kuiweka wazi.
Akiongelea afya yake,Witness ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.
Comments