Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu
waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles
Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea
Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana, na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan
Mshangama.
Mzee
Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye
pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema. Katika mkutano huu wengine
waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail
Semkunde, aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa
mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha.
Mzee
Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia
mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na
kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ya CCM 2010 inavyoendelea.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha juu kadi ya CCM tayari
kumkabidhi Mzee Charles Kagonji ambaye ameorudi CCM kutokea Chadema.
Comments