Nchi za Ufaransa na Iraq leo
wanakutana na kufanya mkutano wa kimataifa mjini Paris ili kukubaliana
kwa pamoja,na pia kuweka mikakati ya kulitokomeza kundi la wanamgambo wa
dola ya kiislam.
Waziri wa mambo ya kigeni nchini
Marekani John Kerry ameeleza kua ameweza kuungananisha takribani nchi
arobaini na zote zimekubali kuingia kwenye muunganohuo zikiwemo nchi za
Kiarab kulikabili kundi hilo nchini Iraq na Syria.
Ushiriki wa nchi za kiarabu katika
mkakati huo kunaongeza nguvu na matumaini ya kupata ushindi wa kampeni
hiyo.wakati huo huo baraza la usalama la umoja wa matifa umelaani vikali
mauaji ya mateka wa kiingereza David Haines aliyechinjwa na kundi hilo
la dola ya kiislam na kuliita tukio hilo kua ni la kuchukiza na la
kikatili mno.
Uingereza mpaka kufikia sasa imechukua
jukumu la kupambana na kundi hilo angani, na Waziri Kerry amethibitisha
kua nchi za kiarab nazo zimethibitisha kujiunga kwenye mashambulizi ya
angani.
CHANZO; BBC SWAHILI
Comments