Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kutangaza siku ya Jumanne
mipango ya kutuma vikosi vya wanajeshi 3,000 nchini Liberia kwa ajili ya
kupambana na virusi vya Ebola, wamesema maafisa wa Marekani.
Inaeleweka kuwa jeshi la Marekani litajenga vituo vipya vya kutolea huduma na kusaidia kuwafundisha madaktari.
Kumekuwa na ukosoaji dhidi ya jumuiya ya kimataifa kupuuzia mlipuko huo.
Siku ya Jumatatu Rais wa Ghana John Dramani Mahama alisema msaada wa
haraka nawa ziada unahitajika na kwamba ungepunguza kusambaa kwa haraka
ugonjwa huo.
Lakini pia Bwana Mahama alisema vikwazo walivyowekewa mataifa ya Afrika Magharibi kumezorotesha mapambano dhidi ya maradhi hayo.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa watajadili majibu ya jumuiya ya kimataifa
dhidi ya mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi kwenye mkutano mjini Geneva.
Comments