Uongozi wa Kenya unasema umefunga madrasa iliyo karibu na mji mkuu kwa kufundisha fikra kali za mapinduzi ya Kiislamu.
Shule hiyo ya dini iliyopo Machakos, karibu kilometa 65 mashariki mwa
Nairobi, ilikuwa imelengwa baada ya baadhi ya vijana wa eneo hilo
kuwekwa kizuizini kwa kushukiwa wanajiunga na wanamgambo wa Somalia.
Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Polisi (CID) ameonya kwamba madrasa hiyo itafungwa.
Kundi la al-Shabab la nchini Somalia limeshafanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya.
Washirika hao wa al-Qaida wanasema wanalipiza kisasi kwa kuwepo na
vikosi vya wanajeshi wa Kenya na nchini Somalia na mauaji ya Waislamu.
Mwaka uliopita, watu 67 waliuawa wakati wapiganaji wa kundi hilo walipoteza na kituo cha duka kubwa la Westgate jijini Nairobi.
Mwandishi wa BBC Abdullahi Abi aliyeko Nairobi anasema ni madrasa ya
kwanza Kenya kufungwa na polisi kutokana na mafundisho yake yenye
msimamo mkali.
Comments