Wayne Rooney amesema aliomba radhi kwa wachezaji wenzake baada ya kutolewa nje dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi.
Nahodha wa Manchester United alitolewa nje kwa kumchezea rafu mbaya
Stewart Downing na kusema hana mpango wa kukata rufaa kwa maamuzi ya
mwamuzi Lee Mason.
“Yalikuwa maamuzi sahihi,” alisema. “ Bila shaka niliomba radhi.”
Man United walishikilia ushindi wao wa 2-1 pamoja na kucheza watu 10 kwenye dakika 30 za mwisho.
Adhabu ya mechi tatu za Rooney zitamfanya akose ‘Manchester derby’ dhidi ya Manchester City Novemba 2.
Naye kocha wa West Ham Sam Allardyce alielezea ukabaji wa Rooney kama
“ukichaa na usio na lazima” wakati kocha wa Man U Louis van Gaal
alikubali kuwa mshambuliaji alipaswa kutolewa.
“Nilimuona mchezaji wa West Ham akitaka kufanya mashambulizi ya
kushtukiza na ndipo nilipojaribu kuyavunja, ila nilikosea kuhukumu,”
alisema Rooney.
Comments