Joseph Kabila
Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila.
Wafuasi
wa upinzani wanataka rais Kabila kuondoka madarakani wakati muhula wake
wa pili wa uongozi utakapomilika mnamo mwaka 2016.
Kuna shaka kuwa huenda katiba ikabatilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.
Maandamano
kwenye mji mkuu Kinshasa yaliripotiwa kuwa ya amani lakini polisi
walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji wa Goma ulio
mashariki mwa nchi hiyo.
Rais Joseph Kabila alichukua mamlaka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa babake Laurent Kabila.BBC
Comments