Liverpool ni moja ya vilabu vinavyofanyiwa uchunguzi kwa kuvunja
sheria za matumizi sahihi ya fedha michezoni (Financial Fair Play (FFP).
Kwa mujibu wa sheria za Uefa, vilabu vyote vinavyoshindana barani
Ulaya lazima vifikie kutumia pauni milioni 35.4 ndani ya misimu miwili.
Kuna adhabu kwa wale ambao hawafikii huko, ikiwemo Manchester City
iliyopigwa faini na kuwekewa kiwango cha kutumia fedha na kiasi cha timu
mwezi Mei baada ya kuvunja sheria.
Ila pamoja na kupoteza pauni milioni 49.8 kwa msimu wa 2012-13 na
pauni milioni 41 kwa msimu wa 2011-12, Liverpool wanaamini kuwa
watafutiwa mashtaka.
The Reds, pamoja na Monaco, Inter Milan na Roma – hakuna kati yao
katika mashindano barani Ulaya msimu uliopita – wamepeleka akaunti zao
kwenye bodi inayosimamia matumizi ya fedha (Club Financial Control Body
(CFCB), ila wameombwa kutoa taarifa zaidi za matumizi yao ya fedha.
Comments