Shirikisho la soka limetuma mkakati wake wa kwanza unaopendekeza
kupunguza idadi ya wachezaji wanaotoka nje ya Ulaya ndani ya soka la
Uingereza kwa asilimia 50.
Kamati ya chama cha FA cha England mapema mwaka huu kilitaka
marekebisho ya jumla yenye imani kwamba wachezaji wengi “wazembe”
walinunuliwa na vilabu.
Agizo hilo la mapendekezo limetumwa kwenye Ligi Kuu, Ligi za soka, na kwa wachezaji pamoja na chama cha makocha.
Chama cha FA kina matumaini kuwa mfumo huo mpya utaanza kufanya kazi msimu wa 2015-16.
Vyama vya soka vya Wales, Scotland na Ireland Kaskazini pia viko katika mjadala na wenzao wa Uingereza.
Mpaka mwisho wa msimu uliopita, wachezaji 122 wa nje ya Ulaya waliingia kwenye soka la Uingereza.
Sheria ya sasa umeutaka mchakato wa GBE (Gvt Body Endorsement)
ulioanzishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani mwaka 2008 kuruhusu serikali
kusimamia maombi ya visa kwa wachezaji wanaotoka nje ya Ulaya.
Comments