Ilikiwa
ni safari ngumu lakini yenye mafunzo mengi nikiwa nimepanda kwenye boti
ya Doria wakati wa msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana na msafara wake tukitokea Nyamisati kuelekea Mafia ambapo katibu
Mkuu huyo yupo katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa
akikagua miradi ya mendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika
shughuli za maendeleo, Nilipangiwa kupanda boti hii ya mwendo kasi ili
kupata taswira za msafara kwa ujumla na hizi ndiyo tawira zenyewe
endelea kuperuzi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-PWANI)
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jamno pamoja na wabunge
wa Mafia Abdulhimid Shah kulia na Abdull Marombwa wakati Katibu wa NEC
Siasa, Itikadi na Uenezi
Nape Nnnauye alipokuwa akiwaaga wananchi katika mji wa Nyamisati wakati
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukielekea Mafia wakati akiwa katikaziara
yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi
kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi
Nape Nnnauye akiwa pamoja na wananchi mara baada ya kupanda kwenye boti
kuelekea kisiwani Mafia jana.(Martha Magessa)
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana na mbunge wa Mafia Mh. Abdulhimid Shah wakipungia mkono wananchi
mara baada ya boti hiyo kuondoka katika pwani ya Nyamisati.
Boti ikikata mawimbi baharini huku bendera za CCM zikipepea.
Mawimbi makali kidogo lakini ndiyo mwendo wenyewe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia
baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo
jana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia
baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo
jana. Katikati anayepunga mkono ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mlao
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi pamoja na mbunge wa Mafia Mh. wakiwa Mafia Mh.
Abdulhimid Shah kwenye pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti
wakati msafara ulipowasili kisiwani humo jana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitoa burudani mara baada ya kwasili kisiwani Mafia jana.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika uwanja wa stendi ya mabasi mjini mafia jana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi jana mjini Mafia.
Mh. Abdulhimid Shah mbunge wa Mafia akiwahutubia wananchi wa jimbo lake.
Naibu
Waziri wa Nishati nishati na madini Mh. Charles Kitwanga akiwahutubia
wananchi wa Mafia na kuwaelezea mipango ya serikali juu ya huduma ya
umeme katika kisiwa hicho.
Comments