Shirikisho la soka la Ghana (GFA) limesema limeacha ushirikiano na
kocha wa timu ya taifa Kwesi Appiah kwa maridhiano ya pande zote mbili.
Kocha wa zamani Milovan Rajevac anatarajiwa kurudi na kuchukua nafasi aliyoishika kati ya mwaka 2008 na 2010.
Rajevan alitakiwa kufanya kazi pamoja na Kwesi Appiah kama mshauri wa kiufundi.
GFA imesema itamtangaza mrithi wa Appiah kabla ya mechi ya kufudhu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea.
Comments