Jitihada
zimeendelea kufanywa katika nchi kadhaa za Afrika magharibi na jumuia
ya kimataifa kupambana na ugonjwa wa ebola ambao umeathiri nchi za
Sierra Leone,Liberia , Guinea hali kadhalika Nigeria kwa kiasi kikubwa
huku Serikali za nchi hizo zikifanya jitihada za kujinusuru na ugonjwa
huo.
Baadhi ya shule Nchini Nigeria zimefunguliwa baada ya
kuchelewa kwa zaidi ya wiki mbili kwa lengo la kujaribu kuzuia
maambukizi ya ugonjwa ebola lakini shule zilizopo mjini lagos ambapo
ndio kitovu cha ugonjwa huo zitaendelea kufungwa mpaka mwezi ujao .
Shirikisho
la walimu nchini humo linaitaka serikali kuchukua hatua ili kuzuia
tishio la maambukizi ya ugonjwa wa ebola kwa wanafunzi, na kusema kuwa
wamesitisha mgomo
Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani (WHO)
limesema kuwa maambukizi ya virusi vya ebola yamedhibitiwa nchini
Nigeria na Senegal miongoni mwa nchi tano ambazo ugonjwa wa ebola umeua
karibia watu 2800.
Raia wa Nchi jirani Sierra Leone walilazimika
kujifungia ndani wa mda wa siku tatu kujinusuru na ebola zoezi ambalo
viongozi wamesema kuwa limefanikiwa.Chanzo ni
Comments