NDOTO
za TP Mazembe kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hii leo
zimeota mbawa baada ya kutolewa na ES Setif ya Algeria kwa mabao ya
ugenini kufuatia sare ya jumla ya 4-4.
Setif
walishinda 2-1 Algeria wiki iliyopita na leo, Mazembe wameshinda 3-2
mjini Lubumbashi- maaba yake timu ya Algeria inakwenda kuumana na AS
Vita ra DRC pia mwezi ujao.
Mabao
ya Mazembe leo yamefungwa na Mghana, Daniel Adjei Nii dakika ya 21,
Salif Coulibaly wa Mali dakika ya 38 na Jonathan Bolingi dakika ya 53,
wakati ya Setif yamefungwa na Abdelmalek Ziaya dakika ya tisa Sofiane
Younes dakika ya 75.Poleni vijana, haikuwa bahati yenu; Watanzania wanaochezea TP Mazembe, Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu kulia |
Comments