Timu ya Liverpool imeendelea na kupata matokeo yasiyo mazuri
katika ligi ya uingereza baada ya wiki iliyopita kupata kipigo cha mabao
3-1 dhidi ya West Ham United na leo imeweza kulazimishwa sare katika
uwanja wake wa nyumbani Anfield na Everton.
Bao la nahodha Steven Gerrad dakika ya 65 lilionekana kuwapa alama
zote Liverpool katika mchezo wa leo .Mchezo uliendelea kwa kasi sana na
mnamo dakika za majeruhi Jagielka wa Everton kutoka umbali wa yadi 30
aliachia bunduki kali sana na kuokoa timu yake na kufanya mchezo kuishia
1-1.
Comments