Jeshi la Nigeria limesema kwamba zaidi ya wanamgambo 260 wa Boko Haram wamejisalimisha kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Msemaji alisema jeshi hilo lilimuua mtu anayechukuliwa kama kiongozi wa kundi, Abubakar Shekau.
Inasemekama Mohammed Bashir ametokea kwenye video ya kundi hilo ila anaonekana kama mtu mwenye sura ya uongo.
Book Haram wameingia hasara kubwa ndani ya wiki za karibuni baada ya
jeshi la Nigeria kupambana na kundi hilo karibu na mji wao wa Maiduguri
kaskazini-mashariki.
Jeshi lilisema kwamba wanachama 135 wa Boko Haram wamejisalimisha
pamoja na silaha zao mjini Biu, kwenye jimbo la Borno – na kwamba
wengine 135 wamejisalimisha maeneo mengine ya kaskazini-mashariki mwa
Nigeria na wanahojiwa kwa sasa.
Mwandishi wa BBC Will Ross aliyekuwepo mjini Lagos anasema kwamba hii haijawahi kutokea katika vita dhidi ya Boko Haram.
Comments