Nahodha wa Nigeria Ahmed Mussa
amesema, soka la sasa halina timu kubwa wala ndogo. Huku akisema kwamba
watu walikuwa wakiipa nafasi kubwa Nigeria ya kushinda kwenye mchezo wao
dhdi ya Stars lakini mambo yamekuwa tofauti
“Mchezo wetu umemalizika vizuri
na sasa uaweza kuona kwamba hakuna timu ndogo wala kubwa kwenye mchezo
wa soka. Watu walikuwa wanasema Nigeria ni taifa kubwa kimpira
ukilinganisha na Tanzania huku wakitupa sisi nafasi ya kushinda mchezo
wa leo lakini mambo yamekua tofauti”.
“Kocha bado anatengeneza timu
yake naamini baada ya mechi kadhaa tutakuwa vizuri japo nimefurahi kwa
jinsi tulivyocheza leo. Kipindi cha kwanza tulishikwa lakini kipindi cha
pili tukacheza vizuri”.Inatoka http://shaffihdauda.co.tz
Comments