Hii
taarifa imegusa Vichwa vya Habari vya Vyombo vingi vya habari Duniani,
inahusu ajali ambayo imetokea wakati watu wakiwa ndani ya Msikiti
Mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia ambako waumini wengi wa Dini ya
Kiislamu huwa wanakwenda kwa ajili ya Hijjah.Ajali hiyo inahusisha winch
kubwa ambalo lilikuwa likitumiwa kwenye ujenzi eneo la jirani na
Msikiti huo kuangukia Msikiti huo, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na
watu zaidi ya 800 wakiendelea na sala ndani ya Msikiti.
Kumekuwa
na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa watu wanaoenda kwenye Msikiti huo
kutokana na maeneo yanayozunguka Msikiti kuna majengo mengi
yanayoendelea kujengwa na kukarabatiwa pamoja na Msikiti wenyewe
kufanyiwa ukarabati wa upanuzi ili kuweza kungiza watu wengi zaidi.
Mpaka
sasahivi Ripoti zinaonesha zaidi ya watu 100 wamefariki, wengine zaidi
ya 200 wamepata majeraha na Mamlaka za Mji huo wanasema sababu hasa za
winch hilo kuanguka inatokana na upepo mkali pamoja na mvua kubwa.http:inatoka //www.mjengwablog.com
Comments