Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza
kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja
Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na Polisi Dodoma
kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri
Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini
Njombe, Lipuli ya Iringa watawakaribisha Kimondo FC Uwanja wa Wambi-
Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa
Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba,
Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja
wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa
kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.
Comments