Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba, baada ya kutolewa katika mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Al Masry huko nchini Misri bado timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Karia Koo inaamini kuwa wao ni mashujaa.
Mashujaa wa kweli!. Simba hatujafungwa bali tumetolewa. Ushupavu wenu, Kupigana kwenu na Uwezo wenu unastahili pongezi…#Tuwapokee mashujaa Dar!.
Simba SC imeyaaga mashindano hayo siku ya Jumamosi usiku baada ya kutoka sare ya bila kufungana na wenyeji wao timu ya Al Masry huko nchini Misri huku mchezo wao wa awali uliyopigwa jijini Dar es Salaam kutoka sare ya mabao 2 -2.
Comments