Halimashauri ya wilaya ya Muheza iliyoko mkoa wa Tanga imeandaa harambee
maalumu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya, wilaya hiyo
ilianzishwa toka mwaka 1974
na ina tarafa 4, kata 37 na vijivi 135 huku ikiwa na vituo viwili tu vya
serikali ambavyo havikizi mahitaji kwa upande wa mazingira na katika
utoaji wa huduma.
Akiongea na vyombo vya habari kuelekea harambee hiyo, mkuu wa wilaya ya
Muheza Mwanaasha Rajabu amesema kuwa tangu alivyoanza Kazi mwaka 2016
amegundua changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo kuwa ni uhaba
wa maji, ukosefu wa ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula
ambapo ardhi kubwa imechukuliwa na watu binafsi kwa ajili ya kilimo cha
mkonge, ubovu wa miundombinu ya Barbara hasa kwa tarafa zilizopo katika
maeneo ya milima na changamoto kubwa ni uhaba wa vituo vya afya.
Aidha amesema kuwa kupitia serikali ya awamu ya tano imejitahidi kufanya
utatuzi wa baadhi changamoto kwa kujenga Barabara yenye kilometa 34
ambavyo itakamilika kufikia mwaka 2020, kuchimba visima takribani 100
katika vijiji mbalimbali, imetoa milioni 30 kwa ajili ya kuvuta maji
mjini na pia rais amefuta hati za mashamba 4 na kuyakabidhi ndani ya
halimashauri ili kuigawa kwa wananchi wenye uhitaji.
Pia ameeleza jitihada zinazofanywa na wananchi katika kufanikisha
shughuli ya ujenzi wa hospitali ya wilaya na kusema kuwa wadau
mbalimbali wamefanikiwa kutoa vifaa vyenye thamani zaidi ya milioni
43.15, serikali imetoa bilioni 2, na halimashauri imetenga bajeti ya
milioni 150 ambapo ujenzi umefanikiwa kuanza kwa upande wa jengo la
wakina mama na jengo la watoto na yapo katika hatua ya msingi na ili
ujenzi wa hospitali nzima ukamilike inahitajika bilioni 11.
Aidha ameweka bayana kuwa kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma ya afya
kwa wananchi, kuchangishana wao kwa wao wameona itachukua mda mrefu
hivyo wameamua kufanya harambee ambayo itafanyika tarehe 16 machi mwaka
huu na mgeni rasmi anatalajiwa kuwa makamu wa rais, Samia Suluh Hasani
na kuongeza kuwa wote wenye mapenzi mema wanakaribishwa katika harambee
hiyo lakini wenye uwezo wa kuto kuanzia kiasi cha milino 1 na kuendelea
na itakayofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden tulip iliyoko
masaki.
Pia ametoa njia mbadala kwa wale wote ambao hawana uwezo wa kutoa
kiwango hicho na kusema kuwa wanaweza kutoa chochote kwa namba ya
kampuni 395533 yenye kumbukumbu namba 123.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments