Dkt. John Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amevionya vyama vya siasa na wananchi ambao wamepanga kufanya maandamo siku za hivi karibuni kwa mujibu wa taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni.
Amesema hayo leo, Machi 9, 2018 wakati akizindua Tawi la CRDB-Bank, Chato mkoani Geita na kuwataka waliojiandaa kutekeleza mpango waache mara mora vinginevyo watashughulikiwa.
“Nchi hii ni ya amani, ndiyo maana uvunjifu wa amani ulipoanza kutokea kule Kibiti tuliamua kuufuta mara moja. Kuna watu wanadhani tunafanya siasa kila wakati, kama wametumwa na baba zao kuandamana, watawasimulia vizuri.
“Wapo Watanzania wachache ambao hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kuambiwa maneno matamu. Mimi niliomba kura kwa wananchi wangu kwa kusema ukweli, nitaendelea kusisitiza ukweli daima,” alisema Magufuli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei ameeleza kwamba uanzishwaji wa Tawi la Benki hiyo Chato ni kutokana na utafiti uliofanywa na Rais Magufuli.

Comments