Mkurugezi wa huduma za uuguzi na wakunga kutoka Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsi,wazee na watoto Gustav Moyo
Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA, Dkt. Sebalida Leshabari
baadhi ya wadau wakiwemo waandishi wa habari waliohudhuria kwenye hafla hiyo
Na Hellena Matale Dar es salaam
Imeelezwa kuwa
wauguzi na wakunga hapa nchini wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo kupatwa na matatizo ya kuumwa mgongo hali inayowafanya washindwe kufanya kazi kwa muda mrefu kama inavyotakiwa.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi
wa huduma za uuguzi na wakunga kutoka wizara ya afya,maendeleo ya
jamii,jinsi,wazee na watoto Gustav Moyo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalojishuhulisha na idadi ya
watu (UNFPA).
Amesema kuwa hapa
nchini bado kuna uhaba wa wakunga na waguzi hali ambayo
imekuwa ikichangia mkunga mmoja kuhudumia idadi kubwa ya
akina mama wajawazito kwa siku bila kupumzika na ambapo hali hiyo imekua
ikiwasabibshia wakunga hao kuiona kazi hiyo kuwa ngumu hata kuchukua
hatua ya kuacha kzai ya ukunga.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA, Dkt. Sebalida Leshabari ameeleza
kuwa kazi ya ukunga ni moja kati ya kazi ambazo zinahitaji moyo
kwani watu wengi hasa wanawake wamekua wakiimbia kazi hiyo kutokana
na mazingira ya kazi kuwa magumu hali ambayo inachangia kuongezeka kwa vifo vya
akina mama wajawazito na watoto.
Ametoa wito kwa
serikali na wadau wa afya kutengeza mazingira mazuri ambayo yanaweza kuwavutia
watu wengine ili waweze kuingia katika kazi hiyo na endapo wakunga wataongezeka
nchini itaweza kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Hata hivyo kongamano
la kisayansi la wauguzi na wakunga linalotarajiwa kufanyika Aprili Nne , tano
na sita mwaka huu mkoani DODOMA mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU.
Comments